Jumatatu 2 Februari 2026 - 21:30
Waingereza walijitokeza mitaani kupinga ukiukaji wa sitisho la mapigano unaofanywa na Israel

Hawza/ Maandamano makubwa yalifanyika jijini London kupinga uuzaji wa silaha unofanywa na utawala wa Uingereza kwa Israel, na pia kupinga ukiukaji usio wa kibinadamu wa sitisho la mapigano unaofanywa na Israel mhalifu.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, makumi ya maelfu ya watu siku ya Jumamosi waliandamana jijini London kupinga ukiukaji wa mara kwa mara wa sitisho la mapigano yanaofanywa na utawala wa “Israel”, ambayo yalianza kutekelezwa tarehe 10 Oktoba lakini limekuwa likikeukwa mfululizo. Waandamanaji hao pia walipinga kuendelea kwa uuzaji wa silaha wa serikali ya Uingereza kuwauzia Tel Aviv.

Kabla ya kuanza kwa maandamano, umati wa watu ulikusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza katika Uwanja wa Russell, London. Waandamanaji walibeba bendera na mabango yenye ujumbe unao ashiria kuiunga mkono Palestina, wakapaza kauli mbiu dhidi ya Israel na serikali ya Uingereza, na waliwataka kwa msisitizo maafisa, makampuni na mashirika yanayouza silaha kuacha kuunga mkono utawala unaotuhumiwa kukiuka sheria za kimataifa.

Maandamano hayo pia yalijumuisha uungaji mkono kwa watu mashuhuri wanaoiunga mkono Palestina, akiwemo John McDonnell na Zahra Sultana, wabunge wa Chama cha Labour cha Uingereza, pamoja na daktari wa Kipalestina mwenye uraia wa Uingereza, Ghassan Abu Sitta.

Maandamano haya yalifanyika sambamba na mashambulizi mapya ya anga ya “Israel” huko Ghaza, ambayo katika muda wa saa 24 yalisababisha kuuawa kwa Wapalestina 37. Kwa masikitiko, utawala huu unaomwaga damu unaendelea kukiuka sitisho la mapigano mara kwa mara. Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Ghaza, tangia kufikiwa kwa makubaliano, majeshi ya “Israel” yamekeuka mara 1450 ukeukahi ambai umesababisha kuuawa kwa watu 524 wa Kipalestina waliodhulumiwa na kujeruhiwa na kuumizwa kwa takribani watu 1360.

Chanzo: Roya News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha